HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » WANASIASA WANAVYOPOTEZA VIPINDI VYA WATOTO SHULE ZA TANZANIA


Na Amini Nyaungo
Mwaka huu wa 2024 una siku za mapunziko 15 siku kuu mbalimbali ambazo zinafahamika kitaifa pamoja na kimataifa, licha ya hayo pia Wanasiasa wa Tanzania wanapoteza muda kwa watoto wa shule kujisomea. 

Wanasiasa wanatumia siasa zao kupita shule mbalimbali kwa ajili ya kueleza mambo yao ya kisiasa ambayo huenda yana maana lakini yanapoteza maana baada ya kuingia katika vipindi na kumwaga sera zao.

Wanawatoa wanafunzi wakiwa katika vipindi kuwasubiri ili waje watoe mambo yao ya kiasasa, ukijumlisha vipindi vinavyopotea kwa ajili ya sikukuu ndivyo unapata picha ya muda unaopotea kuwasubiri wanasiasa na kusikiliza sera zao.

Nilitembelea shule moja katika shughuli zangu za kiuandishi akaja Kiongozi mmoja Mbunge lakini niliona wanafunzi wakamsubiri kuanzia saa tano hadi saa saba mchana.

Hapo ukipiga mahesabu masaa  mawili yamepotea vipindi vingapi vimepotea hapa ?? Ni kweli tunavyotaka Watanzania tuwe na elimu ya juu tutafika kweli ?? 

Hii itaathiri sana matokeo ya masomo mwaka huu 2024 baadae msije mkatafuta mchawi nani juu ya kushindwa kufanikiwa katika elimu.

Wanasiasa msijaribu kutuharibia masomo ya watoto wetu jaribuni kutafuta namna ya kuweza kuwafikia Wanafunzi.

Sio kwamba msifike shule mbalimbali bali mnatakiwa muangalie muda gani unafaa, jaribuni kutafuta muda ambao wamemaliza masomo kisha ingieni kupiga sera zenu.

Najua lengo kubwa ni wazazi wao waende wakawaambie kuwa Mbunge flani amekuja kwa ajili ya jambo flani ila muda mnaoutafuta sio mzuri, watoto wanafeli huko hamjui shida iko wapi ?

Taarifa itakayofuata nitajaribu kuwapiga na picha kabisa ili sasa watu wajue kuwa mnachokifanya sio sahihi ni "UDWANZI" fanyeni siasa kwa utaratibu sio kuwaumiza watoto wetu 

Kwa upande wenu iko vizuri ila kwa watoto wetu  wanaathirika na muda wao pamoja na vipindi vyao kupotea.

Nachoshangaa pia wanapofika eneo husika bado shughuli zenyewe zinaashiria mambo ya chama tena mwalimu naye anahamasisha kabisa juu ya kwa kusema "Amini Nyaungo mitano tena" hapo nimeweka jina langu kuepusha balaa.

Najua hii mtanishambulia ila msumari umeingia mahala pake acheni mambo yenu.

Mwishó 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply