Na Amini Nyaungo
Ligi kuu soka ya Tanzania Bara msimu ulioisha ilikuwa na takwimu za kuvutia sana kwa baadhi ya timu na nyingine kuchukiza kutokana na kile ambacho walichokivuna.
Kwa upande wa Yanga ilikuwa na furaha kwa kuchukua ubingwa pamoja na mafanikio mbalimbali ambayo wameyapata huku Azam FC na Simba SC wakiishia nafasi ya pili naya tatu.
Geita Gold na Mtibwa Sugar wao walikuwa na rekodi mbaya kwani wameshuka Daraja na sasa watacheza ligi Daraja la kwanza.
Leo tunajikita zaidi katika kuangalia takwimu nzima ambazo zilifanyika kwa timu mbalimbali lakini tunaangalia zaidi katika timu tatu za juu ikiwemo Yanga, Azam na Simba.
NIDHAMU
Simba inaongoza kwa nidhamu msimu uliopita kwa kwani imeweza kucheza msimu mzima ikiwa na kadi chache za njano na haikupata kadi nyekundu.
Katika msimu wote haikupata kadi nyekundu hata moja na imepata kadi za njano 28 ikiwa ndio chache zaidi kuliko timu yoyote iliyoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.
Timu inayoongoza kwa kadi za njano nyingi ni Ihefu(Singida Black Stars) ambayo imepata kadi za njano 62 huku DODOMA Jiji ikiwa na kadi 62, Azam FC kadi za njano 51 huku Yanga ikiwa na kadi 36 za njano.
Katika mtitiririko huo kwa ujumla wake kadi zilizotoka kwa timu hizo ni kama ifuatavyo, Singida Fountain Gate 59, Tanzania Prisons 59,Geita Gold 57, Kagera Sugar 50, Namungo 48, KMC 47, Tabora United 44, Mashujaa 43 na Coastal Union 39.
Katika kadi nyekundu timu tatu tu ambazo hazijapata kadi nyekundu msimu ulioishia 2023-2024 timu hizo ni pamoja na Simba, Tabora pamoja na Azam FC.
Hii imeonesha namna Simba sports Club ilivyokuwa na nidhamu katika vipengele viwili vya kadi chache za njano na haikupata kadi nyekundu hizi nyingine zimepata kadi nyingi za njano nidhamu ya Simba inakuja hapo kwa hawa ambao watatu hawakupata kadi nyekundu.
Kwa ujumla wake Yanga wamepata kadi moja ya nyekundu nyingine ambazo zimepata kadi nyekundu moja ni Ihefu,KMC, Kagera Sugar,iliyopata kadi nyingi zaidi ni Ihefu walipata kadi 3 nyekundu.
Jumla ya kadi 23 nyekundu zimetolewa msimu uliopita kwa timu 15 za ligi kuu soka Tanzania Bara swali linabaki msimu ujao itakuwaje ?
Huku kadi za njano 728 zimetolewa kwa timu zote 15 zilizoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania Bara msimu wa 2023-2024.
Kwa aina hiyo Simba imepata nidhamu nzuri sana na huenda kama zawadi zipo za timu zilozokuwa na nidhamu basi Mnyama atapata zawadi hiyo.
REKODI ZA KUVUTIA
Yanga ndio timu pekee iliyopata hati safi nynigi zaidi kuliko timu nyingine ‘CLEAN SHEET’’ nyingi kwa msimu huu ulioisha kwani imepata ‘Clean sheet’ 19 ikifuatiwa na Coastali Unioni yenye clean sheet 16, Azam ikiwa nazo 15 huku Simba ikiwa na 14.
Timu yenye clean sheet chache zaidi ni Mtibwa Sugar yenye clean sheet 5 ikifuatiwa na Singida Foutain Get yenye 7 sambamba na ihefu inayolingana kwa clean sheet.
Yanga inaendelea kutawala eneo hili ikiwa na magoli mengi ya kufunga na machache ya kufungwa ikiwa imefunga magoli 71 na kufungwa magoli 14 ni machache zaidi kuliko yaliyofungwa na watani wao Simba.
Kwa upande wa Simba imefunga magoli 59 na kufungwa magoli 25, Azam FC imefunga magoli 63 na kufungwa 21.
Geita Gold iliyoshuka daraja imefunga magoli 18 na kufungwa 38 wakati huo Mitbwa Sugar nayo imeshuka daraja imefungwa magoli mengi zaidi 54 na kufunga magoli 30.
Jumla ya magoli 497 yamefungwa ndani ya ligi kuu Tanzania Bara na Yanga ndio imechangia magoli mengi zaidi huku kiungo wao Aziz Ki ameibuka kuwa mafungaji bora kwa kufunga magoli 21
Mwisho
No comments: