HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » IDARA YA ARDHI TOENI HATI MILIKI KWA WAKATI KUEPUSHA MIGOGORO-MWIRU

 


Na Sylvester Richard.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Bi Lucia Mwiru ameitaka Idara ya  Ardhi Wilaya ya Singida kushughulikia maombi ya hatimiliki za maeneo yanayofikishwa ofini na wananchi kwa wakati. 


Amebainisha hayo alipokuwa akihitimisha mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Singida uliolenga kujadili utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kusimamia maendeleo  ya Wilaya kuanzia Januari hadi Juni 2024

Aidha, kupitia mkutano huo, Mwiru amemuomba Afisa ardhi Wilaya kushughulikia maombi ya hati miliki ndani ya mwezi mmoja jambo ambalo litaepusha migogoro ya ardhi inayotokana na aidha wananchi kuvamia maeneo yasiyo ya kwao ikiwemo maeneo ya Serikali.
Sambamba na hilo, Mwiru amewaekekeza wakala wa vitambulisho vya Taifa NIDA Wilaya ya Singida kuhakikisha wanaongeza kasi ya utoaji wa vitambulisho kwa waombaji wenye sifa ili wavipate kwa wakati na kuendelea kunufuaika navyo .


Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Mh. Godwin Gondwe amesema kuwa Vijiji 19 vyote vina umeme na imebakia Mitaa michache ambapo amewaagiza Maafisa wa TANESCO kwenda katika Mitaa ambayo bado haijafikiwa na mradi wa umeme wa TANESCO ili wabaini, wombee mradi na wananchi wote wapate huduma ya umeme.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply