Na Amini Nyaungo
Harambee hiyo ilikuwa ya kujengea jengo la Kanisa pamoja na vifaa vya Muziki kwa ajili ya kumsifu Mungu.
Baada ya kupata nafasi ya kutoa neno Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Singida Ambwene Kajula ameomba waumini pamoja na wote waliokusanyika kuwa na na mshikamano katika mambo mbalimbali, licha ya hayo bado ameomba kuacha kujishughulisha na maswala ya ukatili.
"Niombe mshikamano pamoja na upendo baina yetu," Kajula
Aidha, ameitaka jamii kuheshimu na kuwasaidia wazee ili maisha yaende sawa kama ambavyo wao wamewalea utotoni.
"Wazee waheshimiwe walelewe kwani hata sisi walitulea na tuwapende," ameongeza.
Ambwene hakuachilia mbali kuwagusa walemavu akiomba washikwe wasaidiwe na kupewa haki zao huku watoto wapelekwe shule.
Katika harambee hiyo Ambwene ameungana na Mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaa ya Singida Miraji Hamis, Mkuu wa Idara ya Michezo Elineema Babu na Katibu wa SMAUJATA Manispaa ya Singida Hamdun Aboubakar Bui
*Kataa UKATILI wewe ni Shujaa*
No comments: