Na Amini Nyaungo
Hayo ameyasema jana Chief Thomas Mgunto wakati wa uzinduzi wa ligi yake inayofahamika kwa jina la "Cheif Cup" iliyozinduliwa katika shule ya Sekondari Siuyu wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Mgunto amesema kuwa Wilaya ya Ikungi ni kubwa inastahili kuwa na chama cha Mpira wa miguu ili vijana wawe karibu na viongozi wao na kushughulikia kwa karibu mpira wa Wilaya ya Ikungi.
" Nataka tupate chama cha mpira wa miguu hapa Ikungi vijana waweze kushughulikia shughuli za michezo za wilaya hii kwa karibu, " Mgunto.
Katika ufunguzi wa ligi yake Siuyu FC walicheza na Samumba FC ambapo Samumba FC wameshinda magoli 3-2.
Ligi hiyo ambayo imeaza jana itatamatika tarehe 13.10.2024 huku tarehe 14 mwezi huo wa kumi ndio siku ya kutoa zawadi kwa washindi.
Shughuli kubwa waliyoifanya jana kutoa jezi kwa timu zote ishirini pamoja na mipira.
Mwisho.
No comments: