Na Amini Nyaungo
Eliud alitoa ahadi ya kuwapatia jezi pamoja na mipira kituo hiko leo ameitimiza na kuahidi ya kuwa ataendelea kuvisaidia vituo mbalimbali vya soka mkoani hapa.
Wakati wa kukabidhi jezi hizo pamoja na mipira amesema kuwa mpira ni ajira na unaweza ukamtoa mtu kimaisha hivyo anaona watoto wanaweza kubadilisha maisha ya familia zao kwa kuwa na kipaji cha mpira ndio maana hata yeye ameona asaidie vifaa vya michezo kutuoni hapo.
"Niliahidi leo nimetekeleza ahadi yangu, naamini mchezo wa mpira wa miguu unautararibu wake na moja ya vitu muhimu ni vifaa vya kuchezea ndio maana niliahidi na leo nimetekeleza," Amesema
Wakati huo huo amewataka vijana kuendelea kuishi katika ndoto zao na kama wanaamini wanavipaji basi wajikite huko ili waweze kufanikiwa.
Wakati huo Mkurugenzi wa kituo hiko Joseph Mlolele amempongeza mdau huyo huku akiwataka wengine wavisaidie vituo hivyo vifaa vya michezo.
"Ndugu yetu ametimiza ahadi yake nampongeza sana nawaomba wengine wafuate nyayo zake wasaidie vituo vyetu vya michezo, sio hapa tu bali vipo vingi ila kwetu tunamshukuru sana," Mlolele.
Mwisho
No comments: