Na Amini Nyaungo
Moja ya maazimio makubwa na ajenda iliyozungunzwa ni pamoja na Kupinga ukatili wa aina zote kwenye jamii na kuelekeza jinsi ya kuripoti matukio ya ukatili na kuunga mkono juhudi za serikali kwenye kutoa taarifa na kufanya shughuli za maendeleo.
Moja ya maazimio na mkazo kutoka kwa Mwenyekiti Ambwene Kajula juu ya wazee kuweza kuheshimiwa na kulindwa pamoja na kusaidiwa.
Ambwene amesema ya kuwa Viongozi wa SMAUJATA mkoa wa Singida wanatakiwa kuwa na mbinu mbadala ya kuweza kuwakaribisha wananchama wapya wajiunge na SMAUJATA.
Katika kikao hicho amesema kuwa kutakuwa na Kongamano la SMAUJATA mkoani hapa ambalo litafanyika tarehe 28.09.2024.
Uendeshaji wa Kongamano hilo utategemea zaidi na Wananchama juu ya uchangiaji kwa ajili ya kuratibu mambo mbalimbali.
Aidha katika kikao hicho wameelezea juu ya mradi wa kuendeleza SMAUJATA kiuchumi mkoa wa Singida, moja ya michango iliyotolewa ili kuliendea jambo hilo ni ufugaji wa nyuki, Ufugaji wa Mbuzi pamoja na Kuku.
Katika michango ya wajumbe kumependekezwa kuwa na darasa la kutoa elimu juu ya miradi mbalimbali ambayo SMAUJATA Singida wanataka kuyaendea.
Katika kufunga mjadala huu wajumbe wamependekeza Idara ya Uchumi ipokee mapendekezo ya wajumbe na waliyoyapanga wayaunganishe kupata jibu moja la mradi.
*Kataa UKATILI wewe ni Shujaa*
No comments: