Na Amini Nyaungo
Bulugu ameyasema hayo leo wakati SMAUJATA mkoa wa Singida walipokuwa wakifanya mkutano wao wa kila mwezi kama ambavyo maelekezo yalivyoelekezsa kutoka uongozi wa juu.
Bulugu amesema ya kuwa kila kitu kinataka elimu , Mashujaa wanataakiwa wapate elimu juu ya miradi wanayotaka kuitekeleza kisha waingie katika utekelezaji.
Amesema kuwa endapo wataandaa na kupata miradi ya maendeleo hawatohaingaika katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kupinga na kukataza ukatili wa kijinsia.
"Nawashauri muandae mpango kazi wa kuwa na miradi ili mambo yenu yaimarike zaidi wakati sisi huku juu tunaendelea kupambana," Amesema.
Ameshauri juu ya kilimo cha Alizeti pamoja na zao lingine ambalo linaweza kuhimili mkoani hapa.
Singida kuna mazao mengi yanayonawiri moja wapo ni Alizeti, Wele, Mtama, Ufugaji wa nyuki pamoja na Dengu.
*Kataa ukatili wewe ni shujaa*
No comments: