Na Amini Nyaungo, Singida
Siku ya kwanza Mwenge wa Uhuru kupokelewa Mkoani Singida tayari msafara wa Mwenge umetembelea na kukagua miradi 7 yenye thamani ya bilioni 2 Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Katika mapokezi hayo Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amesisitiza Wananchi kuendelea kuungana na wengine kuupokea Mwenge wa Uhuru katika maeneo ambapo utapita.
Mapokezi na makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru yamefanyika katika kijiji cha Kikuyu Wilayani Manyoni mkoani Singida ambapo Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amemkabidhi mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego.
Mkuu wa Msafara wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mnzava amewataka watalaamu pamoja na viongozi mkoani hapa kuwepo katika miradi ambayo wataitembelea huku kuwepo na nyaraka halisi za miradi hiyo.
Mwenge utakimbizwa wilaya zote 5 halmashauri 7 utakabidhiwa Mkoa wa Manyara 12 July 2024 wakati huo kwa Mkoa wa Singida utakimbizwa umbali wa kilomita 800.75.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2024 ni "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu"
Mwisho.
No comments: