Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Nusrat Hanje jana ametoa mifuko ya Cement 100 pamoja na Lori mbili za mchanga katika kikundi cha vijana wanaofanya mradi wa kufyatua matofali cha Chapakazi kilichopo Wilaya ya Ikungi mkoa hapa.
Hanje amesema kuwa yeye ni miongoni mwa Wabunge wanaounga mkono harakati za Rais Samia anazoendelea kuzifanya katika kuwakomboa vijana na wananachi wake.
Wakati anakabidhi Mifuko hiyo ya cementi ameweka wazi kuwa ataendelea kushirikiana nao vijana katika kila zuri watakalolifanya ili mradi waendelee kufanikiwa katika maisha yao.
"Tutaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali kama kuna jambo zuri tutashirikiana ili tija upatikane," Hanje.
Hanje ametumia nafasi hiyo kuwaomba vijana kubuni mbinu mbalimbali zitakazoweza kuwaletea maendeleo pamoja na kipato ili waendeleze familia zao.
"Jitahidi kubuni miradu utakayoweza kuwasaidia kiuchumi kama ambavyo mradi huu unafanyakazi, " Hanje.
Aidha Mbunge Hanje amewapa nauli vijana zaidi ya 200 ambao walimaliza na kufunga kambi yao ikiwa na lengo la kuwafikisha majumbani mwao.
Kwa upande wa vijana waliokabidhiwa msaada huo wamefurahishwa na kuendelea kuwaomba wengine waige mfano wa Nusrat Hanje katika kuwaunga mkono vijana.
Mwisho
No comments: