Na Amini Nyaungo
Mwenge wa Uhuru kwa mkoa wa Singida mwaka 2024 utapitia miradi 47 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 100.121 ambapo utakimbizwa katika wilaya tano za mkoani hapa pamoja na Halmashauri zote 7 utapokelewa July 5,2024 na utakabidhiwa July 12 kwa mkoa wa Manyara.
Hayo ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Singida MH. Halima Dendego alipokuwa anaongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake juu ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ambapo utapokelewa shule ya Msingi Chikuyu katika kijiji cha Kikuyu kilichopo Wilaya ya Manyoni saa kumi na mbili asubuhi akitanabaisha kuwa maandalizi yamekamilika na kuwaomba wananchi kujitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru.
"Maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani Singida yamekamilika,niwaombe wananchi wajitokeze kwa wingi kuupokea," Dendego
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni "Kutanza Mazingira na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na maendeleo endelevu ya taifa".
" Niwaombe Wanasingida tushirikiane kwa pamoja kuona mbio hizi za aina yake na umuhimu wake," Dendego.
Mheshimiwa Halima Dendego ameishukuru serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha Shughuli mbalimbali za maendeleo, huku akimsifu kwa kutumia vyema Diplomasia kupelekea wawekezaji na wahisani kujitokeza na kuwekeza nchini Tanzania.
Aidha katika kutunza mazingira amesema kuwa Singida ina kila sababu ya kuweka mazingira safi na salama katika mipango yao wanaendelea kupanda miti na mwaka huu wamepanda miti milioni 9.75 pia wameweka mikakati ya kuitambua miti ya asili.
Kwa kutambua umuhimu wa vyanzo vya maji Mwenge wa Uhuru utapita katika vyanzo mbalimbali vya maji mkoani Singida .
"Sisi tunashiriki kutunza mazingira kama ilivyo sehemu nyingine za dunia, tunaendelea kuhamasisha watu kutumia nishati safi ya kupikia, kauli mbiu yetu Singida ya Kijani ndio dira yetu,"Dendego
Aidha katika hali ya usalama amewahakikishia wananchi kuwa watakuwa na tahadhari huku akiwashauri wazazi kuwa makini na watoto kwani ulinzi wa awali unaanzia kwao ila wao kama serikali wataimarisha ulinzi.
Mwisho
No comments: