Na Amini Nyaungo
Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Singida Ambwene Kajula jana 16.07.2024 alitoa elimu ya ukatili wa kijinsia mkoani hapa katika mkusanyiko wa mkutano wa Injili uliofanyika kata ya Mtipa.
Katika nafasi aliyopata Kajula aliwaambia waumini ya kuwa ukatili wa kijinsia upo kila mahali hivyo kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake kumlinda asifanyiwe ukatili huku akitaka amani ya nchi iendelee kama ilivyo sasa ili waumini na jamii ipate kumjua vizuri Mungu.
"Ndugu zangu tunafanya ibada bila shaka wala woga kwakuwa tuna amani tusikubali kuvuruga amani tuliyonayo, kama hakuna amani hii basi hata ibada zenyewe hazitokuwa vizuri,"Kajula
Aidha amewaomba wazazi kuwa karibu na watoto wao kuangalia mienendo yao kwani wao ndio waathirika wakuu katika maswala ya kufanyiwa ukatili.
"Niwaombe wazazi na waumini tujiangalie na tuwe walinzi sisi wenyewe pamoja na kuwalinda watoto wetu kwani wao ndio waaathirika zaidi wa ukatili, tukipata kuwaangalia watoto wetu tutaweza kuwa salama kwenye familia zetu," Kajula.
Mwisho
No comments: