HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » SABE WAWASHIKA MKONO WENYEMAHITAJI MAALUM IRAMBA

 

Na Amini Nyaungo 
Shirika lisilo la Kiserikali SABE lililopo Iramba Mkoani Singida limetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa watoto wenye uhitaji maalumu. 

Hayo yamefanyika tarehe 09.07.2024 wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani Singida yaliyofanyika Wilaya ya Iramba ambapo Mkurugenzi wa Shirikia la SABE Mr. Samson Benard amesema wametoa kwa moyo na amewaomba wahisani wengine wajitokeze kuwasaidia wenye uhitaji.


" Tumekuja kutoa msaada huu ili kuwawezesha vijana wenye uhitaji wajihisi wako sehemu salama," Alisema

Miongoni mwa vifaa walivyovitoa ni pamoja na Madaftari, Viti vya wenye ulemavu, Peni, Penseli , Bima ya Afya kwa watoto 42 na vitendeakazi vingine vyenye thamani ya milioni moja laki mbili na Ishirini natano.

Kwa upande wake Katibu wa SABE Miriam amesema kuwa wataendeea kuwafariji watu mbalimbali katika kuleta usawa kwao nawao wajihisi wako katika nchi yenye amani.

Aidha amewaomba watu mbalimbali kuungana nao kuwasaidia watu wasiojiweza.

"Nichukue fursa hii kuwaomba watu wenyekujiweza wawasaidie watu wenye mahitaji maalumu," Miriam.
Katika tukio hilo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka huu Godfrey Mnzava amewapongeza wadau na wahisani wote waliotoa misaada kuwasaidia wenye uhitaji. 

Mwisho. 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply