Yanga na Simba ndio timu zilizo na wafuasi (mashabiki )wengi Tanzania kila sehemu wanapoenda kucheza mechi wao wanakuwa wenyeji hata kama ikiwa mikoani.
Timu hizi zimejitengenezea utaratibu wao mzuri wa kuendelea kuvuna mashabiki na sasa wameanza kunufaika nao kwa kuwawekea utaratibu wa kuwatambua kwa kuwapa kadi na kuzilipia klab zinanufaika na ada zao za mwaka.
Yanga na Simba wamekuwa wakichukuliana wachezaji kwa taabu sana katika hao wengine wamekuwa wakifanya vizuri na wengine wakishindwa kuonesha kile ambacho kipo vizuri.
Ibrahim Ajibu
Zao la vijana la Simba kizazi chao kilifanya vizuri sana na baadae wakapandishwa kuchezea timu kubwa ya Simba.
Wengi waliamini kuwa Ajibu ana kipaji cha hali ya juu sana uhodari wa kutoa pasi za mwisho, kufunga na kuuchezea mpira. Wengi hawajaamini baada ya usajili wake kutoka Simba kwenda Yanga, licha ya kuwa kipenzi cha Mohamed Dewji ambaye ni Muwekezaji wa timu hiyo lakini alitoka na kusakata kabumbu Yanga ila baada ya msimu mmoja alirudi Simba.
Ajibu amefanikiwa zaidi akiwa Yanga kwa msimu huo ambao alijiunga nao amesaidia kufunga magoli 8 na kutoa pasi za mwisho 15 hajawahi kufikia rekodi hiyo hadi sasa hivi katika maisha yake ya mpira na mshambuliaji tegemeo wa Yanga wakati huo ni Heritier Makambo alifunga magoli ya kutosha kwa pasi za mwisho za Ajibu.
Mrisho Ngassa
Ngassa moja ya mawinga machachari sana kuwahi kutokea katika ardhi ya Tanzania mafanikio makubwa ameyapata akiwa Yanga baada ya kutoka Kagera Sugar 2006 inasadikika kuwa ni mshabiki wa Yanga kwa maneno yake mchezaji mwenyewe.
Ndiye mfungaji bora wa muda wote timu ya taifa ya Tanzania amefunga magoli 25 ambapo wachezaji wanaomfuatia kwa ufungaji ni Msuva na Samatta wote wakiwa na magoli 22. Amepata bahati ya kupita vilabu vitatu vikubwa hapa Tanzania akianzia Yanga kisha Azam FC na baadae akaenda kwa mkopo Simba ila kote huko hakufanya vizuri zaidi alipokuwa YangĂ .
Vilabu alivyowahi kucheza Ngassa ni pamoja na Kagera Sugar, Yanga, Simba, Azam FC, Free State, Fanja FC na Mbeya City, aliwahi kufanya majaribio Westham United ya England chini ya kocha Franco Zola ila alifeli.
Jonas Mkude
Moja ya wachezaji waliokuwa na rekodi nzuri sana ndani ya ligi kuu bara, mafanikio zaidi ameyapata akiwa Simba ndiye mchezaji ambaye ana makombe mengi kuliko wote waliopo ligi kuu Tanzania Bara.
Ameibukia Simba ya vijana 2011 na 2012 wamechukua ubingwa wa ligi kuu Bara, hadi sasa amechukua ubingwa mara 6 akiwa na Simba pamoja na mara moja Yanga, amechukua kombe la Shirikisho mara nne mara moja akiwa na Yanga huku akichukua mara tatu akiwa Simba.
Amecheza "Kariakoo Derby" 32 nyingi zaidi ya mchezaji mwingine yoyote huenda hata huko zamani mafanikio zaidi ameyapata akiwa Simba.
Clatous Chama
Yanga wamemtambulisha Clatous Chama kuwa ni mchezaji wao na hawajasema mkataba wa muda gani japo tetesi zinasema mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine kama akifanya vizuri.
Katika misimu mitano aliyohudumu Simba amecheza michezo 139 ya ligi kuu Bara amefunga magoli 27 ametoa pasi za mwisho 54 wakati huo katika michuano ya inayoendeshwa na Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) amecheza michezo 44 amefunga magoli 15 na kutoa pasi za mwisho 6.
Swali ni kwamba je Chama ataonesha makali yake kama aliyoyaonesha Simba ? Hilo linabaki kuwa swali ambalo jibu lake hadi msimu utakapoanza na kama akionesha makali yake ?
Baadhi ya wachezaji wengine waliowahi kucheza Yanga na Simba kwa muongo mmoja na nusu uliopita ni pamoja na Amir Maftah, Amri Kiemba, Hassan Dilunga, Kelvin Yondani, Nurdin Bakari, Ramadhan Waso, Emenuel Okwi na Juma Kaseja.
WALIOFELI KINA NANI ?
Juma Kaseja
Jina hili ni kubwa mno hapa nchini Tanzania alicheza kwa mafanikio akiwa Simba alifika kuwa kipa namba moja Tanzania kwa wachezani wa ndani yaani "Tanzania one" .
Usajili wa kutoka Simba kutua Yanga haukuwa wa kawaida kwani nguvu nyingi zilituma lakini hakuwa kuwa bora kwa msimu mmoja ambao amechezea Yanga kifupi alifeli Yanga.
Emanuel Okwi
Nyota Raia wa Uganda kipenzi cha mashabiki wa Simba aliitesa sana Yanga marehemu Yusuph Manji ameweza kumshusha Jangwani ili aisaidie timu yake, kwa bahati mbaya hakucheza kwa kiwango ambacho walitarajia huyu naye alifeli.
Kufeli kwao kwa Kaseja na Okwi sio walifeli mpira bali hawakucheza katika kiwango bora wakiwa Yanga lakini baadae walitafuta njia nyingine na walifanya vizuri, Okwi alirejea tena Simba alikiwasha sana, Kaseja naye akatafuta maisha mengine akakiwasha sana.
No comments: