Na Amini Nyaungo
Mrakibu wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Singida Devota Bigawa amesema kuwa matukio ya majanga ya moto kwa upande wa zimamoto yako vizuri huku akiwashauri wananchi kutoa taarifa mapema ili kusaidia kuyakabili matatizo hayo.
Ameshauri wananchi kutoa taarifa mapema pindi majanga ya moto yanapotokea ili wapate usaidizi mapema pamoja na kuwakaribisha wananchi kufika ofisini kwao kuweza kupata elimu pamoja na kuweka miundombinu ya nyumba vizuri.
Aidha amesema kuwa moja ya changamoto wanayoipata kutopata taarifa mapema wakati majanga yanapotokea.
"Wahanga wanachelewa kutoa taarifa mara tu baada ya kupata majanga ya moto, nawashauri wapige snu kwa wakati ili tukauzime kwa wakati," Bigawa
Pamoja na miundombinu kutokuwa rafiki katika sehemu wanazoenda kuzima moto wananchi wametakiwa kujua kuwa zimamoto wanapofika wanatakiwa kuangalia uelekeo wa upepo ppamoja na mambo mengine ya kitalaam.
Wananchi wametakiwa kupiga namba 114 katika matumizi sahihi kwani kuna badhi ya watu wanaitumia namba hiyo vibaya.
"Watumie bamba 114 kwa usahihi kwani wengine wanatumia kwa kufanya masikhara, hivyo nawamba wapige pindi wanaokuwa na matatizo," Bigawa
Mwisho.
No comments: