HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » ASKARI WANAPOTAMBULIWA NA KUPEWA TUZO, WANAONGEZA ARI KATIKA MAJUKUMU YAO

 Na Sylvester Richard

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP Amon Daudi Kakwale amesema kuwa askari wanapotambuliwa na kupewa vyeti vya pongezi na tuzo baada ya kufanya vizuri katika utendaji, wanaongeza ari na katika majukumu yake.

Amebainisha hayo Juni 27, 2024 Makao Makuu ya Polisi  Singida alipokuwa akitoa vyeti vya pongezi na tuzo kwa askari 7 waliofanya vizuri kwenye utendaji mwaka 2024.
Aidha Kakwale amesema, utoaji wa zawadi hizo ni kwa mujibu wa PGO namba 37. ambayo inalitaka Jeshi la Polisi kuwatambua askari waliofanya vizuri na kuwapa tuzo.

" *Kwa mujibu wa PGO yetu namba 37 inatutaka kama ilivyo kwa watumishi wengine kuwatambua na kuwatunuku Wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kila mwaka kwa kufanya kazi vizuri"* amesema Kakwale.


Ameongeza kwa kuwaasa askari kufanya kazi kwa weledi na kamwe kutokuwa sehemu ya wahalifu.


Akiongea kwa niaba ya waliopata vyeti na tuzo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Jacob Jairos Mgwama amemshukuru Kamanda kwa kumuongoza vyema na yeye kuyatii maelekezo aliyokuwa akimpa kupitia wasimamizi wake wa karibu hadi kupata zawadi hizo.


Amewaasa askari wengine kuongeza jitihada   na kufikia malengo ya Jeshi la Polisi ambayo ni kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao unaimarika. 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply