HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » » IPI KALI KATI YA TIMU HIZI ZA SINGIDA ?

Mkoa wa Singida umebahatika kupata timu za kuiwakilisha mkoa na timu hizo ni Singida United, Singida Big Stars na Singida Black Stars kwa nyakati mbalimbali. 
Kimsingi Singida United ndio kongwe kuliko hizi mbili, ilipanda daraja mwaka 2000 na ikashuka mwaka huo uliofuata ilipita miaka 20 bila ya kuwa na timu hadi pale ilipopanda tena daraja kuiwakilisha Singida. 

Singida United ilipopanda tena ilifanya  vizuri kwa kiasi kikubwa mmiliki wa timu alijitahidi kuchagua wachezaji walio na viwango vya hali ya juu sana ikawa tishio katika timu zilizo za daraja lake. 
Singida United ilifanikiwa kufika tano bora ligi kuu Tanzania Bara bado kama haitoshi ilifika fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup kwa sasa inaitwa CRDB Bank Federation Cup fainali ilipigwa Arusha ikaukosa ubingwa mbele ya Mtibwa Sugar. Timu hii ilitoa wachezaji wengi ambao walisalia ligi kuu Bara baada ya kushuka daraja. 


Katika harakati za kurudisha amani mkoa wa Singida ikaibuka timu ya  bank moja DTB ilivyopanda daraja basi ikawa furaha kwa Wanasingida baada ya fununu za muda mrefu kuwa timu hiyo itakuja mkoa wa Singida na "Don" mmoja ataifikisha hapo.

Ni kweli ilivyopanda ikabadilishwa jina na ikaitwa Singida Big Stars usajili uliofanyika kila mmoja ameuona, Duke Abuya, Tchakei, Kagere,  Khomein , Wawa, pamoja na nyota wengine waliounda Singida Big Stars timu hii imefika nne bora na ikacheza michuano ya kombe la Shirikisho msimu wake wa kwanza ilisumbua na wachezaji wake kama vile Bruno ambaye alikuwa mfungaji bora wa timu hiyo.

Mauzauza yalianza mara baada ya kubadilishwa tena jina ikaitwa Singida Fountain Gate FC wengi walitarajia huenda ikawa moto wa kuotea mbali msimu huu ikawa na madeni ya kufa mtu ilibidi baadhi ya wachezaji wahamie timu nyingine, kumbe mchezo unachezwa nje ya chaki tetesi za kuchukuliwa Ihefu na kusimikwa kuwa katika mji wa Singida zilianza.

Baadhi ya nyota kama vile Tchakei, Abuya, Khomein, Rupia wote wakahamia Ihefu kampeni ikawa kuipambania timu hiyo isishuke daraja, na ikawezekana na hivi sasa nayo inaitwa Singida Black Stars.

Swali langu linasalia pale pale ya kuwa ipi timu kali kati ya hizi tatu Singida United, Singida Big Stars na Singida Black Stars? Kwakuwa hatuwezi kuihukumu Singida Black Stars kwakuwa "Don" ameichukua katikakati ya msimu ila tunaweza kuongea kitu kwa usajili ambao wanaufanya.

Kipekee maua yaende kwa skauti anayehusika kuangalia wachezaji wanaokuja Singida maana yupo vizuri anachagua wachezaji wa kiwango cha hali ya juu sana pengine hata mapacha wa Kariakoo hawawezi kuwafikia kwa jicho lao.

Baada ya mashabiki wa mpira mkoa wa Singida wameweza kutoa maoni yao juu ya mjadala huu wa ipi timu kali kati ya Singida tatu.

Dafi Nyandekwa yeye ni Mwenyekiti wa Stend kuu ya mabasi Misuna mkoani hapa, amesema kuwa Singida United ndio ilikuwa kali zaidi kwani ilifika hadi fainali ya shirikisho na ilisumbua sana wakati wake.

"Kwangu naona Singida United ndio ilikuwa timu ya mauaji ilifanya vizuri sana na ilifika hatua ya fainali kombe la Shirikisho la Azam, ilikuwana wachezaji hodari sana," Alisema.

Andrew Kipaji yeye ameona Singida Big Stars ndio ilikuwa bora zaidi kwani ilifika hatua ya kucheza michuano ya kombe la Shirikisho la Soka Afrika lakini pia imefika nne bora ligi kuu bara.

"Ile United ilikuwa kali lakini hii Big Stars imefika mbali imetuwakilisha kimataifa kwa mara ya kwanza na imetinga nne bora katika ligi ya ndani," Amesema 

Mohamed Makiya yeye ameona hizi Singida mbili zote zilifanya vizuri  ila anaaubiria aone moto wa Singida Blac Stars ikianza msimu mpya.

"Zote zilifanya vizuri ila tusubiri hii Black Stars ikianza msimu najua itaongeza wachezaji," Makiya.

Je wewe ipi unaoina Singida Kali kati ya hizo tatu.

Mwisho.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply