HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » SERIKALI IMEWAJIBIKA KUTENGENEZA BARABARA ZILIZOATHIRIKA NA EL NINO

 Serikali imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 136.2 kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) na Wakala ya Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), kwa ajili ya kurejesha hali ya awali ya miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibiwa kwa kiasi kikubwa na janga la mvua za El Nino.


Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali 2024/2025.

Dkt. Mwigulu amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa.

Amezielekeza Taasisi zote zinazohusika na ujenzi wa miundombinu kuhakikisha zinafanya usanifu wa miradi kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi.

Amesema kufuatia mvua za El-Nino zilizonyesha nchini kuanzia Septemba, 2023 pamoja na kimbunga Hidaya, barabara mbalimbali za kitaifa katika mikoa 26 zimeathirika ambapo barabara 68 zilikuwa zimejifunga, barabara 106 zilikuwa zinapitika kwa shida na barabara 168 ziliathirika lakini zinaendelea kupitika kwa shida baada ya kufanyiwa matengenezo ya dharura.

Amefafanua kuwa shilingi bilioni 184.14 ni kwa ajili kurejesha miundombinu iliyoathiriwa na kimbunga Hidaya.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply