HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » WATUMIENI POLISI KATA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA WA MAENEO YENU


Na Sylvester Richard




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP Amon Daud Kakwale amewataka viongozi wa Serikali za Mitaa kuwatumia Polisi Kata katika kuimarisha ulinzi na usalama wa maeneo yao kwa kutoa taarifa za wahalifu kwa usahihi na kwa wakati.


Alisema hayo Mei 3, 2024 alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya watu wa Manispaa ya Singida wakiwemo viongozi wa Serikali za Mitaa, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa

madhehebu ya dini, wazee wa kimila na wamiliki wa makampuni ya ulinzi binafsi kwenye kikao  kilichofanyika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida.


Sambamba na hilo, Kamanda Kakwale aliwasisitiza wajumbe wa kikao hicho kushirikiana kikamilifu na Jeshi la Polisi katika kubaini kuzuia na kutanzua uhalifu kwa wakati na kwa njia salama.


Kikao hicho ambacho pia Kamanda Kakwale amekitumia kujitambulisha, kilikuwa huru na wazi ambapo wajumbe walipata nafasi ya kutoa kero na kuchangia hoja mbalimbali zilizolenga kuimarisha ulinzi na usalama wa Mkoa wa Singida.



Naye  Mstahiki  Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu ambaye pia alihudhuria kikao hicho,  alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kupeleka huduma ya Polisi kwenye Kata na kusema kuwa Polisi kata wamekuwa msaada mkubwa kwa jamii kwakuwa uhalifu umekuwa ukipungua siku hadi siku ambapo aliliomba Jeshi la Polisi lishirikiane na Mshauri wa Mgambo Wilaya katika kuwafundisha vijana wenye sifa juu ya ulinzi shirikishi ili vijana wafanye kazi ya ulinzi kwa uelewa zaidi.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply