HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » ASKARI WATAKIWA KUKATAA RUSHWA KILA MAHALI.*

 


Na Sylvester Richard



Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga amewataka askari wa Mkoa wa Singida kukataa rushwa kila mahali wanapokutana na watu wasio waaaminifu wanaotaka kuwahadaa na  kuwapa rushwa ili wafanye udanganyifu wa kesi mbalimbali.


Mganga amesema hayo Mei 3, 2024 katika hotuba yake aliyoitoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida aliyealikwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye Hafla ya kumuuga Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida DCP Stella Alchard Mutabihirwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa RC Mission Manispaa ya Singida.



Aidha, Dkt. Mganga amewasisitiza askari kutosheka na mishahara yao na kuepuka kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo ya nchi na ya mtu mmoja mmoja.



Kwa upande mwingine, amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuiombea Nchi ili iendelee kuwa na amani na wananchi wake waishi katika maadili.

Akiwaaga askari wa Mkoa wa Singida, DCP Mutabihirwa amewashukuru askari na wananchi wa Mkoa wa Singida kwa kushirikiana vyema tangu alipoingia Mkoani humo akiwa na cheo kidogo hadi alipoondoka na cheo cha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) huku akiuacha Mkoa ukiwa shwari.


Naye Kamanda wa Polisi wa sasa wa Mkoa wa Singida SACP Amon Daudi Kakwale ambaye pia amepokelewa rasmi katika hafla hiyo ameahidi kuendeleza mazuri aliyoyafanya DCP Mutabihirwa wakati akiwa Kamanda wa Mkoa huo.


Hata hivyo, Kakwale amewaomba askari na wananchi wa Mkoa wa Singida kumpa ushirikiano katika kubaini, kupambana na kutanzua uhalifu ili Mkoa wa Singida uendelee kuwa shwari.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply