HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » FARM RADIO WAANDAA MAUDHUI YA VIPINDI VYA KILIMO

  


Msimamizi Miradi wa Farm Radio International(FRI) kwa upande wa Tanzania Susuma Susuma amewaomba wakulima kutumia vizuri Radio wanazopewa na Taasisi hiyo ili wapate elimu inayolengwa kila mradi unapoanza.


Hayo ameyasema leo mkoani Dodoma katika Semina ya Kilimo iliyofanyika katika Ukumbi wa African Dreams Hotel ambapo  lengo lilikuwa ni kuandaa Maudhui ya vipindi vinavyohusu kilimo ambapo vitakavyoruka katika Radio za Singida na Dodoma, kwa upande wa Singida ni Standard Radio huku Dodoma Mwangaza FM.

Susuma amesema lengo la kuwapa Radio wasikilize vipindi mbalimbali ikiwemo wanavyorusha katika mradi wao wa kilimo cha Ikolojia kupitia Radio ambazo wamezichagua.

"Mkawaambie wakulima wazitumie vizuri hizi Radio zinauwezo mkubwa lakini lengo letu wapate elimu tunayoitoa kupitia Radio washirika wakipata elimu wazifanyie kazi ziwasaidie katika kilimo chao," Susuma


Semina hiyo ilihusisha Waandishi wa habari, Maafisa Kilimo, Wakulima pamoja na Wadau mbalimbali kama vile Mkulima Mbunifu ambao nao wanahusika katika maswala ya kilimo. 

Naye Mkuu wa kitengo cha Radio wa Farm Radio International Ester Mwangabula amesema kuwa lengo la Semina hiyo ni kuwajengea uwezo Wakulima, Waandishi pamoja na Maafisa Kilimo wanapoenda kutekeleza mradi huo wafanye vizuri kama ambavyo wameelekezana.


"Tumewaita hapa kwa ajili ya kuwawakilisha wakulima wenzetu lakini muende mkafanye vizuri mradi huu wa kilimo ili Wakulima waweze kuelewa na kulima kilimo chenye tija," Mwangabula


Kwa upande wake mkuu wa Kitengo cha Tehama Caroline Kimaro ametoa mrejesho wa kitengo chake namna kilivyofanya msimu mliopita pamoja na namna wakulima watakavyowasilisha mada zao kupitia "Uliza Polls'' na watangazaji watazitumia katika vipindi vyao vya mradi huo.


Maafisa Kilimo, Wakulima na Waandishi wa Habari kwa siku ya kwanza wameweza kuandaa vipindi 12 ambavyo miongoni mwa vitakavyoruka katika radio hizo mbili.

Farm Radio International (FRI) inasambaza miradi mbalimbali ya kilimo kwa Radio za Tanzania ikiwa na lengo la kuwapa elimu Wakulima juu ya kilimo bora chenye tija.

Mradi huu ni wa ambao utakaoanza mwezi wa sita mwaka huu 2024 ni miaka mitatu utakaohusisha mikoa miwili ya Dodoma na Singida na utazungunzia Kilimo cha Kiikolojia, kilimo ambacho hakina madhara kwa mtumiaji wa mazao yanayozalishwa na kilimo hicho.

Mwisho 

 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply