HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » TUMIENI MIZANI KUUZA BIDHAA ZENU-WILLE

Wananchi wa Mkoa wa Singida wametakiwa kutumia vipimo katika biashara zao wanazouza kila siku ili kutenda haki kwa wateja wao pamoja na wao wenyewe kutokujipunja. 


Hayo ameyasema Afisa Vipimo mkoa wa Singida Wille Amos alipowatembelea wafanyabiashara mkoani hapa ambao wanatumia njia ambazo sio za halali za kuuza bidhaa zao kama vile Vitunguu, Nyanya pamoja na Mahindi kwa kutumia visado,Kimbo na ndoo za Lita ishirini. 


Wille amewaomba  kuanza kutumia mizani na kuacha kutumia Visado, Kimbo pamoja na Plastiki pia amewapa ushauri kuwa wanaweza kuunda  vikundi na wakanunua mzani watakaoweza kuutumia kwa ajili ya Shughuli zao za kila siku. 

" Nawaomba mtumie mizani hii itawasadia nyinyi kutoa haki kwa mteja na nyinyi wenyewe kutokujipunja,"Wille


Wille ametembelea soko la Unyakindi ambalo wanauza bidhaa za Nyanya pamoja na Mahindi, soko la Msufini pamoja na soko la Kimataifa la vitunguu lilipo Misuna mkoani Singida ambapo kote huko ametoa elimu hiyo ambapo kwa kiasi kikubwa walielewa na kuahidi kuanza kutumia mizani. 


Aidha baada ya kutoa elimu aliwapa nafasi ya kuuliza maswali pamoja na kutoa maoni yao juu ya elimu aliyoitoa juu ya matumizi ya mizani.


Ali Yusuph muuzaji wa mahindi ambaye anatumia debe kupimia amemuahidi Afisa Vipimo kuwa watajitahidi kununua mizani ili itumike katika shughuli zao za biashara.

"Nimekuelewa mimi nitatumia mizani katika shughuli zangu , kwa sasa najipanga na nashukuru kwa elimu hii," Amesema.

Mfanyabiashara wa nyanya Aisha Juma amesema kuwa licha ya wao kuelimishwa wanatakiwa waendelee kutoa elimu ili wananchi waelewe zaidi. 

"Tumepata hii elimu lakini tunaomba muendelee kutoa elimu zaidi ili watu waelewe na tutumie mizani," Aisha

Wiki ya vipimo dunia inaazimishwa tarehe 20 ya kila mwaka ambapo kwa mkoa wa Singida wataazimisha kwa aina yake ikiwemo kutoa elimu kwa watu mbalimbali.

MWISHO. 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply