HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » TUTAKUTIBU UTARUDI KUJIBU KERO ZA WANANCHI- MAKONDA



Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda amewaasa viongozi wa ngazi mbalimbali mkoani humo kuwa tayari kujibu kero za wananchi wao katika siku sita za ziara yake itakayofanyika huanzia tarehe 23 Mei 2024.



Makonda amesema kuwa kiongozi yoyote atakayeumwa wakati wa kujibu hoja za wananachi watamtibia hospital akipona atajibu hoja zao ili kila mmoja abakie salama.

Makonda ameziita siku sita za moto katika ziara yake akiahidi kuwa na tahadhari ya kila kitu ikiwemo gari za kubebea wagonjwa, Helicopter na vifaa vingine ili kuokoa watu watakaopata matatizo wakati wa mikutano yake.

Amesema kuwa yeye anahitaji kuweka alama kwa siku atakazokuwa madarakani sehemu yoyote atakayoenda huku akiwaonya viongozi waliopata nafasi kwa kupitia vimemo watanyooka au waamue kufanyakazi vizuri. 

Ziara yake itakuwa ya siku sita ya kusikiloza kero mbalimbali za wananchi na kuweza kuzitatua.

Makonda aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akiteuliwa na Rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete kisha utawala wa Magufuli aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam hadi alipogombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni ndipo ukawa ukomo wa uongozi wake kabla ya Rais Samia kumpa kazi ndani ya Chama ya kuwa Katibu wa Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baadae akateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambayo bado yupo hadi hivi sasa.

Mwisho. 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply