HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » MIGOGORO YA FAMILIA SABABU YA KUINGIA KATIKA URAIBU

 Jamii imeaswa kuacha kugombana katika familia zao ambapo hiyo inapelekea baadhi yao kujiingiza katika kutumia Dawa za  kulevya ambayo ni hatari anayeingia atachukua muda mrefu kurudi katika hali ya kawaida. 

Hayo yamesemwa jana DKT Christian Mbwasi Afisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kutoka Ofisi ya Kanda ya Kati  alipo fanya mahojiano na Standard Radio juu ya madhara ya matumizi ya Madawa za kulevya katika Jamii. 

Mbwasi ameweka wazi kuwa yoyote anayetumia Dawa za kulevya itachukua muda mrefu kurudi kama aivyokuwa zamani hivyo jamii wajilinde wenyewe na kuzilinda familia zao. 


" Kwa yoyote aliyeingia kutumia madawa ya kulevya mara nyingi huku kuna mlango wa kuingilia ila hakuna wa kutokea, niwaombe familia kutokuwa na migogoro ya hapa na pale kwani hii ni sababu moja wapo ya watu kuingia katika matumizi ya dawa za kulevya," Mbwasi. 

Aidha amesema watu wanaotumia dawa za kulevya kiafya wako hatarini kwani kuna uwezekanao mkubwa wa kuambukizana virusi vya ukimwi kutokana na kutumia bomba moja la sindano lakini pia homa ya Ini pamoja na kifua kikuu.

DKT Mbwasi amesema kuwa watu ambao wameingia katika  matumizi ya dawa za kulevya wanatakiwa wasaidiwe ili warudi katika hali zao za kawaida na waweze kuzalisha ndio maana wanatoa elimu kupitia Radio na sehemu mbalimbali.

"Walioingia katika dawa za kulevya wanatakiwa wasaidiwe ndio maana hatua ya kwanza tunatoa elimu ili waachane na uraibu lakini pia tunawapeleka Soba kwa ajili ya matibabu," Ameongeza.

Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply