HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » TAKUKURU SINGIDA WASISITIZA KLABU ZA WANAFUNZI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imehamasisha vyuo na shule mbalimbali mkoani hapa kuwa na Klabu za wanafunzi wanaopinga na kukataza Rushwa ili elimu hiyo ipatikane kila mahali. 

Akizungunza siku ya leo katika kipindi cha Zinduka cha Standard Radio Mtoa elimu kutoka Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Singida Joseph John ameweka wazi kuwa swala la kuzuia na kupambana na Rushwa la wote hivyo kila mmoja anastahili kuichukia Rushwa, ndio maana wanataka kila shule na vyuo kuwe na klabu za wanafunzi wanaokataza Rushwa. 


" Tuna sisitiza kuwepo na Klabu za wanafunzi kutoka shule mbalimbali na vyuoni wanaokataza Rushwa ili kila mmoja apate kuguswa na hili naamini elimu hii ikianzia shuleni itakuwaa rahisi hata wanapoingia kazini baada ya kumaliza shule, " John. 


Pia amesisitiza kuwa na kosa kutoa na kupokea rushwa na kuwataka wananchi kuripoti maswala yote yanayohusu Rushwa ofisini kwao kwa ajili ya kuyafuatilia, huku akisema kuwa taarifa zozote wanazozipata ofisini kwao zinakuwa siri baina ya mtoa taarifa na ofisi ya TAKUKURU.

Mwisho.. 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply