Kufuatia tamko la Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu alipotembelea Tasisi ya MOI kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan atagharamia matibabu ya upasuaji na utengamao kwa watoto 100 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Nchini familia ya Samsoni Salamba wakazi wa Kata ya Tinde Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameiomba Serikali kumsaidia huduma ya matimbabu mtoto wao mwenye umri wa miaka mitatu ambaye anasumbuliwa na tatizo hilo.

Wakizungumza na Chember media kwa nyakati tofauti wazazi wa mtoto akiwemo baba mazazi Samsoni Salamba amesema mtoto amezaliwa na tatizo hilo ambapo walielekezwa na wataalamu wa Afya kuwa wafike Hospitali ya Bungando kwaajili ya matibabu Zaidi lakini hawakufanikiwa kupata huduma kamili kwasababu ya ugumu wa maisha hivyo wakaiomba serikali iwasaidie kwa uapande wa matibabu ili mtoto aepukane na ulemavu huo na aendelee kupata haki zake za msingi hasa elimu ili atimize ndoto zake.
Viongozi wa Serikali akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Igalamya Ferister Bundara amesema Serikali kupitia mfuko wa Tasafu katika kusaidia kaya masikini viongozi walishindwa kumsajili katika mfumo wa Tasafu kwasababu hakukidhi vigezo vilivyohitajika huku Mtendaji wa Kata ya Usule Shimba Waziri amesema familia inatumia nguvu kubwa katika kumhudumia mtoto hali ambayo inawazorotesha kiuchumi na kushindwa kupata mahitaji sitahiki.
Waziri wa Afya, Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametoa tamko hilo Aprili, 21, 2024 alipotembelea Taasisi ya MOI kwa ajili ya kuwajulia hali watoto 25 waliofanyiwa upasuaji chini ya ufadhili wa MO Dewji Foundation ambapo amesema kuwa amepewa maagizo na Raisi Samia Suluhu Hassani kutoa fedha kwaajili ya matibabu ya watoto miamoja wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi huku akiwataka akinamamawanaotarajia kupata ujauzito wafike Vituo vya Afya mapema ili wapate huduma sitahiki.
Mwisho
Post a Comment