HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » TRA SINGIDA WATOA ELIMU YA UMUHIMU WA KUTOA NA KUDAI RISITI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  mkoa wa Singida jana wametoa elimu juu ya kutoa na kudai risiti sahihi kwa mteja na mfanyabiashara ili kuisaidia serikali kukusanya mapato yake kwa njia rahisi isiyokuwa na misuguano.


Hayo ameyasema jana Afisa elimu kwa Mlipakodi na mawasiliano  wa TRA Swaumu Mvungi katika kituo cha Radio juu ya  umuhimu wa matumizi ya mashine za kutolea risiti (Electronic Fiscal Device) EFD, Electronic  Tax Stamp(ETS) na (Vitual Fiscal Device) VFD. 

Amesema kuwa mfumo wa utoaji risiti ulianzishwa ili kuboresha utunzaji wa kumbukumbu za biashara ameongeza kuwa kuwepo kwa mfumo huo utasaidia kuwepo kwa uwazi baina ya mlipa kodi na Taasisi ya Kodi (TRA) na kuondoa migongano ya kikodi baina ya Mlipa Kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

"Mfumo huu umetolewa ili kuboresha  utunzaji wa kumbukumbu za biashara, uwepo wa mfumo huu utasaidia uwazi baina ya mlipa lodi na Mamlaka ya mapato," Swaumu.


Katika elimu aliyoitoa amesema mteja anaweza akafahamu risiti aliyoipata kuwa ni halali pamoja na , tarehe na muda halisi ya mauzo, Kiasi au Gharama hakisi cha pesa kilichonunuliwa bidhaa au huduma pamoja naTIN na jina la mnunuzi. 

Aidha ameongeza kuwa mteja atafahamu kuwa stempu halali inakuwa na nenmbo ya TRA ikiwa ina namba na Alphabet(Alphanumeric) pamoja kua na mng'aro. 

Swaumu amesema kuwa kwa yoyote anayekiuka utaratibu atakapobainika anapewa faini  kupitia sheria ya usimamizi wa kodi kifungu cha 86 kupitia kifungu kidogo cha 1-4 kwa muuzani asie toa risiti faini ni 20% yabthanani ya mzigo au huduma au Shilingi Milioni moja na elfu hamsini(1,500,000) huku mnunuzi aliyeshindwa kudai risiti faini 20% ya kodi iliyokwepwa au Shilingi elfu thelathini (30,000).

Mwisho.. 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply