HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » JAMII IMEASWA KUACHA KUWATUHUMU WAZEE KUWA NI WACHAWI

 

Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Manyoni Juma Amrani amewaasa wakazi wa wilaya hiyo kuacha imani potofu za kishirikina kwa kuwatuhumu  wazee kuwa ni wachawi na wengine inafikia hatua ya  kuwadhuru katika masha yao.

Amrani amewataka kusitisha mara moja kuwatishia wazee hao kuwa ni wachawi kwani haileti picha nzuri huku akisema kuwa kijana wa leo ndiye mzee wa kesho. 



Hayo ameyasema leo walipokuwa katika kikao cha dharula cha kutatua mgogoro wa Wananchi ambao wamemtuhumu mama ambaye umri wake mkubwa pamoja na watoto wake wawili kuwa ni wachawi ambapo waliwataka wahame katika kijiji hicho.



Baada ya tukio hilo Mashujaa na wakiongozwa na Amrani  wakishirikiana na watuhumiwa wameripoti polisi ambapo baada ya taarifa hiyo polisi waliwashikilia watu sita ambao walifanya tukio hilo la kuituhumu familia hiyo na baadae kupewa kifungo cha nje.


" Tumeenda Polisi kwa ajili ya kuripoti katika vyombo vya dola na wameweza kutupa ushirikiano mzuri hadi sasa watu sita wameshikiliwa na polisi," Amrani.



Licha ya watuhumiwa kukamatwa Amrani amesema kuwa ushirikiano wa Jeshi la polisi pamoja na Hakimu wakishirikiana na mchungaji kuweza kupata maridhiano baina ya familia hiyo na watuhumiwa.


" Watuhumiwa Walienda kituo cha police kutoa taarifa na watuhumiwa walikamatwa wakiwa 6 na kufikisha mahakamani tunashuru jeshi la police itigi kwakuonyesha ushirikiano na Mheshimiwa Hakimu wa Mahakama ya mwanzo Itigi tunawashukuru sana maridhiano  ilisimamiwa na baba mchungaji pamoja na sisi SMAUJATA Wilaya ya Manyoni na mwenyekiti wa Chilejeo na wajumbe wa kitongoji na wazee maarufu   na Wanakitongoji kwa ujumla, " Ameongeza. 

Amrani amewaomba wananchi kuhofia Mungu kwani kila kitu kipo katika vitabu wasichukue sheria mkononi.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply