HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » BIZY TECH MKOMBOZI KWA WAKULIMA SINGIDA NA DODOMA



Kampuni ya Bizy Tech leo imetoa mafunzo ya mradi wa kilimo kwa Maafisa Kilimo, Wakulima na wadau mbalimbali wa kilimo juu ya Kilimo bora ambacho chenye tija katika jamii mafunzo hayo yamefanyika mkoani Singida ambao utadumu kwa miaka miwili ambapo kwa awamu hii itahusisha mikoa ya Dodoma na Singida.



Meneja wa kampuni hiyo George James Olwak amesema kuwa kampuni yao inatoa mafunzo ya kilimo  kutumia Mtandao pamoja na ushauri ikiwa na lengo la kuwasaidia Wakulima kulima kilimo bora chenye tija na kiwasaidie katika maisha yao. 

George ameweka wazi kuwa Tech inaendelea kuelemisha jamii kuhusu mambo makuu mawili katika kilimo Kushauri juu ya Kilimo bora pamoja na kuwasaidia katika kujua hali ya hewa, lakini kupitia mfumo wao wa kilimo bora wataweka katika huo mfumo wa kilimo bora Application kupitia huo mfumo hata aliyekuwa na simu ya kawaida atapata taarifa. 


"Tunamfikia mkulima kwa njia mbalimbali ili kuboresha kilimo na kuboresha mahitaji ya mkulima mmoja mmoja, kwa kipindi hiki tumekuja Singida na Dodoma kuwaletea mradi unaitwa kilimo bora ambao unatoa ushauri kwa mkulima, tunatoa ushauri juu ya udongo bora ambapo sisi Bizy Tech tunampimia bure tunakuja na vifaa vyetu baada ya kupima tutamshauri Mkulima alime nini atumie mbolea ya aina gani  lakini pili sisi Bizy Tech tunashirikiana na Mamlaka ya Hali ya hewa ili mkulima ajue mvua zinaendaje na mambo mengine," George 


Bizy Tech itasaidia mkulima kujiunganisha na soko ili akilima awe na uhakika wa soko.


Aidha amewataja washirika wa kampuni hiyo ni pamoja na GSMA,Serikali ya Jamhuri ua Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya kilimo,Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Mamlaka za seriali za Mitaaa.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply