Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani amewataka Vijana Mkoani Singida waliopo katika Vyuo na Shule za Misingi na Sekondari kuanzisha Miradi ya Kilimo (Bustani) pamoja na Ufugaji katika Maeneo ya Shule na Vyuo walinaposoma.
Ndahani ameyasema hayo leo wakati wa ziara ya kugakagua Miradi ya Vijana wa Skauti katika Vyuo,Shule za Msingi na Sekondari alipoifanya katika Chuo cha Maendeleo (FDC) Singida.
Ndahani amesema ni wajibu wa uongozi wa vyuo na Shule kutenga maeneo maaluumu watakayo tumia Vijana katika kujifunza na kuendeleza kilimo na Ufugaji katika Shule na Vyuo kwasababu Shule nyingi Mkoani Singida zina maeneo ya kutosha lakini hayatumika katika uzalishaji au Mafunzo ya Kilimo au Mifugo ambayo inasababisha watu kuyavamia maeneo hayo na kuanzisha migogoro ya Shule na Wananchi.
" Ni muhimu vyuo kutenga maeneo kwa ajili ya vijana kujifunza kilimo, Singida kuna maebei mengi sana," Amesema
" Kwa kufanya hivi tutakuwa tumesaidia Vijana wetu kupata uzoefu na kupenda kulima na kufuga badala ya kukichukia kilimo," ameongeza.
" Katika Nchi yetu ipo fursa kubwa katika Sekta ya Kilimo na Ufugaji na Serikali imeweka Mazingira Mazuri ya Vijana katika kilimo ambapo Serikali hutoa mbolea ya Ruzuku Nchi nzima pamoja na Mbegu ya Alizeti ambayo ndiyo zao Kuu la Biashara katika Mkoa wetu," Ndahani.
Suphiani Nurduni ambaye ni Kiongozi wa kundi la Skauti Tawi la Chuo cha FDC amesema wameamua kujikita katika kilimo cha Mboga kwasababu kuna fursa kubwa ya kibiashara katika mboga kwa kuwa kila familia na Wanachuo huhitaji Mboga kwa ajili ya Chakula hivyo amesema licha ya kupata kipato Vijana wanakuja na kujifunza kilimo cha Mboga Mboga hapa katika vitalu.
Mkufunzi wa Chuo Samwel Isaya Tarimo ambaye ndiye Msimamizi wa Shughuli za Kilimo na Ufugaji chuoni amemushukuru Afisa Vijana Mkoa kwa kufanya ziara na kutembelea Shughuli za Kilimo na mifugo inayotekelezwa katika Chuo cha FDC.
Mwisho.
Post a Comment