MTUMISHI UKIPEWA ZAWADI INAYO ZIDI ELFU HAMSINI IPELEKE KWA BOSS WAKO-JOHN TAKUKURU

Mtumishi anapopewa zawadi inayozidi elfu hamsini anatakiwa aipeleke kwa mwajili wake ili ampe risiti  au aiamulie matumizi mengine ya pesa hiyo kwaajili ya ofisi.

Hayo ameyasema leo Joseph John Kailanya Afisa kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Manispaa ya Singida alipokuwa anaongea na Standard Radio katika kipindi cha asubuhi juu ya kwanini watu wanatoa na kupokea Rushwa. 


"Muajiliwa yoyote akipata zawadi baada ya kufanyakazi vizuri anatakiwa aipeleke kwa muajili wake ili ampe risiti na aiamulie matumizi mengine au ampe yeye aliyepewa, " John. 

John ametumia fursa hiyo kuelezea kwanini watu wanatoa rushwa akisema ni mmonyoko wa maadili kwa wanaotoa na wanaopokea. 

Mwisho. 

Post a Comment

Previous Post Next Post