Ofisi ya BAKWATA Mkoa wa Singida kupita sheikh Mkuu wa Mkoa wa Singida Issa Bin Nassoro amezipongeza Taasisi za Ramadhani Charity Program 2024 na JAI kwa kutoa sadaka Magereza ya Manispaa ya Singida.
Hayo ameyasema leo katika ziara yake ya kutembelea Wafunguwa kwenye Gereza la Manispaa ya Singida nakutoa Sadaka Iftar kwa Wafungwa kwa ajili ya kupata Futari pamoja na daku ambapo Sadaka hizo zimetolewa na Taasisi za Ramadhani Charity Program 2024 pamoja na JAI.
Sheikh Issa awaomba watu mbalimbali kuwajali watu wenye Mahitaji na Masikini nijambo jambo ambalo linampendeza Mungu hata mitume walifanyia wema watu masikini.
"Napenda kutoa Rai kwa waumini wezaangu tupende kutoa Faraja na Sadaka ya Iftar kwa makundi kama haya hii leo tumetoa, kwani kunawaumini wezetu wapo humu na wanamahitaji mbalimbali hasa katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani, " Sheik Issa
Sheikh Issa ametumia fursa hiyo ya kuzipongeza Taasisi ya Ramadhan Charity Program 2024 pamoja na JAI kwa kujitoa na kuwasaidia watu wenye mahitaji katika Mkoa wa Singida.
Ramadhani Charity Program 2024 ikiongozwa na Ahmed Missanga kwa kushirikiana na Taasisi ya JAI wametoa sadaka ya Iftar mbalimbali katika Magereza Manispaa ya Singida mahususi kuwajali watu wenye mahitaji maalumu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Ramadhan Charity Program 2024 Ahmed Misanga amesema wamemua kushirikina na Bakwata mkoa kutoa Sadaka Iftar huo kwaliji ya jamii ya wafungwa walioko Magereza waweze kupata dauku na futari katika kumi la Mwisho la Ramadhani.
Kupita Progmram hiyo wameza kuwapatia wafunguwa Sadaka ya sukari mchele unga tambi Maharange na tende pamoja taulo za kike kwa Ajili ya wafungwa wakike.
Lakini pia Taasisi hizo zimetoa Tende kwenye Ofisi ya Sheikh Mkuu wa mkoa Singida kwa ajili ya wahudumu wa Ofisi hiyo katika kipindi hichi cha Ramadhani.
Huku upande wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Ramadhan Charity Program 2024 Ahmed Misanga Amesema huu ndio utaratibu wao wa kila mwamka wakutoa Sadaka Iftar kwa watu wenye maitaji Hasa Magereza na Mkundi Mengine heye uhitaji.
Hata ivyo misanga alisisitiza kwamba watu waliopo magerezani wanahitaji huruma ya watu waliopo Uraiani ili wawe na faraja nakumjua mungu ili wanapo rudi Uraini wawe watu wemaa.
Mkuu wa Gereza Hilo SP Yusuph Athumani Amesema Amefuraishowa na Tasisi hiyo kwa kuapatia Sadaka Iftar kwani uatawasaidia sana.
"Tutatuima hii Sadaka Iftar kama milivyo kusudia na tuombea kwa mungu awalipe pale mlipo toa kwa ajili ya wafugwa wote wakike na wakiume," amesema
Taasisi hiyo inafanya harakati za kutoa Sadaka Iftar kila mwaka na mwaka huu tayari imetoa misaada kwa mikoa mitano na inaendelea kutoa hadi mwisho wa mwezi mtukufu.
Mwisho.


Post a Comment