PACOME, AUCHO , YAO WAPO TAYARI KUIVAA MAMELODI

 

Nyota wa tatu wa Yanga walioikosa Mamelodi Sundowns katika mkondo wa kwanza Yao Kousi, Pacome Zouzou na Khalid Aucho wapo tayari kuwavaa Masandawana katika mchezo wa mkondo wa pili utakaochezwa Afrika ya Kusini wiki hii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kupitia "App'' yao wameweka wazi kuwa nyota wao wote watakuwepo katika kikosi kitakachoenda Afrika ya Kusini. 

Wachezaji hao ni pamoja na makipa, Djigui Diara, Metacha Mnata na Aboutwalib Msheri, mebeki Kibwana Somari, Bakari Nondo, Ibrahim Bacca, Dickson Job na Joyce Lomalisa, Nickson Kibabage na Gift Fred.

Huku viungo ni pamoja na Maxi Nzengeli, Khalid Aucho, Salum Aboubakari , Jonas Mkude, Mudathiri Yahya na Zawadi Mauya

Viungo washambuliaji, Pacome Zouzou, Aziz Ki, Okrah, Farid Mussa, Denis Nkane na Skudu Makudubela.

Washambuliaji ni pamoja na Joseph Guede, Kenedy Musonda na Clement Mzinze.

Tarehe 05.03.2024 Yanga atarejean na Mamelod ambapo mchezo wa kwanza waitoa sare ya bila kufungaa mbungi iliyopigwa uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam. 

Post a Comment

Previous Post Next Post