MANYONI WAENDELEA KUPOKEA MISAADA KUTOKA RAMADHANI CHARITY PROGRAM



Taasisi ya Ramadhani Charity Program 2024 chini ya Mwenyekiti Mohamed Missanga imetoa msaada wa Box moja la tende kwa Sheikh wa walaya ya Manyoni kwa ajili ya wasaidizi wa ofisi ya Sheikh wa wilaya hiyo.


Tasisi hiyo kwa kushirikina na Jamali Juma imewapatia msaada kina mama wajane mchele, Sukari, Mafuta, unga,  pamoja na pesa za mboga. 


Missanga awataka wajane kuwa na umoja na kupendana ili watimize ndoto zao za kimaisha kwa kufanya kazi pamoja na biashara ndogondogo na kuwa karibu na Mungu.



Taasisi hiyo inafanya harakati za kutoa misaada hii kila mwaka na mwaka huu tayari imetoa misaada kwa mikoa mitano na inaendelea kutoa hadi mwisho wa mwezi mtukufu. 


"Tunaendelea kutoa misaada kadri tutakayojaaliwa," Misanga


Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post