Bank ya CRDB leo limeingia mkataba wa miaka 3 na Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) wa kuidhamini michuano ya shirikisho hilo hafla iliyofanyika ofisi za bank hiyo jijini Dar es salaam.
CRDB wameingia mkataba wa miaka 3 utakaokuwa na thamani ya Bilioni 3.76 kuanzia hatua ya 16 bora ambapo michuano hiyo ipo hivi sasa.
Msimu huu CRDB watatoa kiasi cha shilingi milioni 255 kama sehemu ya udhamini katika msimu huu .
Michuano hii ndio ile ambayo ilikuwa inadhaminiwa na Azam iliyofahamika kama Azam Sports Federation Cup ambapo kwa sasa itafahamika kama CRDB Federation Cup.
Upande wa CRDB umewakilishwa na Mkurugenezi mtendaji wa Bank hiyo Abdulmajid Nsekela huku TFF alikuwepo Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia wakati wa kusaini mkataba huo.
Baada ya zoezi hilo kukamilika Rais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania Wallace Karia ameweka wazi kuwa viwanja vitakavyotumika kuchezea nusu fainali ni CCM Kirumba Mwanza na Tanzanite kilichopo mkoa Arusha.

Post a Comment