Chama cha mpira wa miguu Manispaa ya Singida (SIDIFA) kikiongonzwa na Katibu wake Jonas Dani leo wamefanya kikao chao cha kwanza juu ya kozi ya ukocha ya 'Grassroots' kozi ya wiki moja ambayo inatarajia kufanyika mwezi Mei 27,2024.

Jonas amewaomba wapenda soka wote mkoa wa Singida wajiunge na kozi hiyo kwani ni muhimu sana kwa mpira wa miguu mkoani hapa.
"Hii kozi ni muhimu sana kwa makocha mpira unahitaji soka lenye kueleweka maana hii grassroots ni soka la vijana, tutarajia kuanza kozi hii mwishoni mwa mwezi Mei" Amesema
Katika kikao hicho cha kwanza kimeweza kueleza gharama ya kozi hiyo ni shilingi laki moja.
"Gharama ni laki moja, hivyo tujitahidi tupate watu thelathini," Jonas.
Jonas ametumia fursa hiyo kusema kuwa hakuna kocha atakayeruhusiwa kukaa kufundisha mpira bila ya kuwa na kozi ya ukocha ya Grassroots au kozi nyingine za mpira.
" Nitumie fursa hii kuwaambia kuwa bila ya kuwa na kozi ya ukocha kuanzia ligi daraja la nne lazima awe na kozi ya ukocha," Ameongeza.
Lakini pia ametoa ufafanuzi endapo watu watazidi zaidi ya thelathini darasa litagawanywa kikubwa ni kutoa michango na wale waliokuwa tayari.
Katika kikao hicho kimehudhuliwa na Abuu Majojo ni "General Coordinator" wa SIREFA naye amewashauri wote waliokuwa tayari wajiunge na kozi hiyo kwani ipo nyumbani.
Baada ya kikao hicho wamechagua viongozi wa watakaoongoza katika darasa la kozi hiyo ni pamoja na Hamis Stone yeye akiwa Mwenyekiti akisaidiwa na Amini Nyaungo huku Hamis Mgusi akiwa mweka hazina wa darasa hilo.
Mwisho.
Post a Comment