MWENYEKITI WA SMAUJATA SINGIDA AWEKA WAZI MAPATO NA MATUMIZI




Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Singida Ambwene Kajula amethibitisha uwazi na ukweli katika uongozi wake baada ya kutoa taarifa ya kiasi cha pesa kilichopatikana  za michangoya shughuli iliyofanyika Mwankoko mkoani Singida pamoja na matumizi yake.

 Taarifa yake ambayo ameituma katika kundi la Whatsapp ameanza kuwashukuru Mashujaa kwa kaI nzuri ksiha chini kuweka wale ambao wamechanga na namna ilivyotumika.

Taarifa hiyo ya Mwenyekiti inasomeka kama ifuatavyo chini.

" Habari za jioni wapendwa Mashujaa! 
Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu kwa makuu aliyotutendea katika kufanikisha jambo letu la Mwankoko.

Nawapongeza na kuwashukuru sana kwa jinsi mlivyojitolea kwa hali na mali kuhakikisha tunafanikisha shughuli yetu ya Mwankoko namuomba Mungu awazidishie sana na awabariki kwa makuu mnayoyafanya. 

Naomba pia niweze kuwaletea taarifa fupi ya mapato na matumizi katika shughuli yetu na mafanikio.

*A. Michango iliyokusanywa katika maandalizi ya shughuli ya mwankoko*

1. Ambwene Stephen Kajula 50,000
2. Rajabu Athumani 24,000
3. Ally Dude 10,000
4. Godfrey Mbua 10,000
5. Irene 30,000
6. Linda Nguma 24,000
7. Almacheus Mwita 24,000
8. Mohamedi Shabani 24,000
9. Hawa Ntandu 20,000
10. Juma Maftaa 24,000
11. Ashura Athumani 24,000
12. Mariamu Amos 5,000
13. Semeni Chamresha 10,000

*Jumla 269,000*

*B. Matumizi ya fedha iliyokusanywa*
1. Matangazo 60,000
2. MC 100,000
3. Usafiri wa Matent na Viti 55,000
4. Ulinzi 4,000
5. Mapambo 50,000

*Jumla ya matumizi 269,000*

*C. MAFANIKIO*
1. WATOTO WATATU  WALINUNULIWA KADI ZA *NHIF*
2. ELIMU MBALIMBALI ZILITOLEWA kama:-
       A. Elimu ya Smaujata
       B. Elimu ya ukatili
       C. Elimu ya ukeketaji
       D. Elimu ya Sheria 
     
3. Maendeleo yaliyofanywa na Mh Rais Dr Samia Suluhu Hassan
4. Pongezi kwa mazuri ambayo serikali imeyafanya kupitia Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassani 
5. Mgeni Rasmi Mstahiki Meya na Viongozi wengine wa Chama na Serikali. 

Narudia kwa kusema *asanteni sana* kwa ushirikiano Mkubwa mliotupatia. Hakika huu ni upendo Mkuu kwa Smaujata.

*Asanteni sana namuomba Mungu awabariki sana.*

Mwisho... 

Post a Comment

Previous Post Next Post