Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Singida Jesca Kishoa jana ametekeleza ahadi yake aliyoitoa siku ya Jumamosi kwa wananchi wa Kata ya Ibaga Wilaya ya Mkalama mkoani hapa.
Kishoa aliahidi kutoa milion tatu la laki mbili ili kumalizia ujenzi wa Zahanati ya IBAGA ambayo imejengwa kwa nguvu za Wananchi wa eneo hilo.
Jana amekabidhi kiasi cha milioni tatu na laki mbili Kwa uongozi wa eneo hilo huku akitarajia hatua za ujenzi zianze mara moja ili Wananchi wapate huduma.
"Niwashukuru kwa kunikaribisha na mapokezi mazuri mliyonipa naamini nina deni zaidi ya hili tuendelee kuwa pamoja ninatoa kiasi hiki kwa kuona umuhimu wa jambo hili namie niungane nanyi kujenga Hospital hii, "Kishoa
Baada ya tukio hilo la kukabidhi pesa Kishoa aitembela ofisi ya Kata pamoja na Kituo cha polisi na kuahidi kushirikiana nao katika kusaidia yale yanayowezekana.
Mwisho


Post a Comment