TBN WAWAJIA JUU WATABIRI WA MCHONGO MTANDAONI

 TBN WAWAJIA JUU MANABII WA MCHONGO MTANDAONI



Na Mwandishi Wetu



Wamiliki wa Blog nchini Tanzania (TBN) umelaani vikali vitendo vya watu mbalimbali kufanya utabiri kisha kusambaza katika mitandao ya kijamiii wakitabiri mambo ya nchi ambapo vitendo hivyo vinakiuka Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Hayo yamezungunzwa jana August 11, 2025 jijini Dar es Salaam katika kikao kazi cha mafunzo ya mabloga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ambapo washiriki walikubaliana kuchukua msimamo wa pamoja kulinda maadili na weledi wa mawasiliano mtandaoni.



Mabloga hao wamezitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kushirikiana kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wote wanaojihusisha na vitendo hivyo, wakisisitiza umuhimu wa kutekeleza sheria bila upendeleo.


Aidha, kikao hicho kilibainisha uwepo wa kundi la watu wanaojiita manabii, ambao wamekuwa wakitoa kauli zinazokiuka sheria za nchi na kuibua taharuki kuelekea uchaguzi mkuu. Baada ya kupitia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Personal Data Protection Act), washiriki walihitimisha kuwa tabia ya kutoa utabiri wa aina hiyo ni uvunjifu wa haki ya msingi ya faragha ya wananchi.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post