USAID AFYA YANGU SINGIDA WAADHIMISHA SIKU YA KIFUA KIKUU KWA NAMNA YAKE

 


Wananchi wa mkoa wa Singida wameaswa kupima  afya zao mara kwa mara ili wajue kama wanaumwa magonjwa mbalimbali.


Hayo yamesemwa leo na Aminiel Wilfred  Mfinanga Afisa Vifaa na Takwimu Idara ya Elimu Sekondari manispaaa ya Singida akimuwakilisha Athuman Hemed Mnyusi Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Singida ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi. 


Aminel ameweka wazi kuwa uchunguzi wa ugonjwa wa TB unafanyika bure hivyo wananchi wafike katika vituo vya afya ili wapatiwe huduma. 


Kwa upande wake Meneja Mradi wa USAID Afya yangu kwa mkoa wa Singida Dokta Said  Mgeleka amewataka kila mmoja aliye na ugonjwa wa kifua kikuu apelekwe akapimwe ili apatiwe dawa bila hivyo maambuzi ya ugonjwa huo utaendelea kusambaa


Ugonjwa wa kifua kikuu uligundulika kwa miaka 140 iliyopita Dar es Salaam nchini Tanzania na mazimisho ya kitaifa yatafanyika mkoa Dodoma hapo kesho.

Mwisho. 

Post a Comment

Previous Post Next Post