SENDIGA AONGEA NA WAZAZI MANYARA

 Na Saulo Steven, Manyara

MANYARA.



Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga amewataka wazazi na walezi kuweka kipaumbele na kuhakikisha watoto wao wanakuwa chini ya uangalizi wao katika kipindi chote cha sikukuu.


Sendiga ameyasema hayo leo ofisini kwake Wakati akizungumza na Standard Radio huku akawakikishia wananchi wote wa Mkoa wa Manyara juu ya kuimarishwa maradufu kwa Ulinzi na Usalama katika kipindi hiki cha mapumziko ya sikukuu ya Pasaka.



Mkuu wa mkoa wa Mnayara Queen Sendiga

Amesema kuwa pamoja na mikakati ya kiusalama iliyowekwa lakini wananchi wanapaswa kuhakikisha familia na mali zao zinawekwa kwenye mazingira salama.


Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema kuwa kama hakuna ulazima wa kwenda sehemu za starehe basi ni vyema wananchi wakasherehekea Pasaka majumbani kwao kwa amani na utulivu huku akiwatakia wakristo na Wana Manyara wote heri katika sikukuu ya Pasaka.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post