Ili kulinda maadili na nidhamu Walimu nchini watakiwa kubadilika na kulinda maadali kwa watoto wa mashuleni hii itawasaidia kuwa katika wakati bora wa maadili kwa watoto wao.
Hayo yameelezwa jana na Sheikh Mkuu wa Wilaya Singida ISSA BIN SIMBA wakati wa ufunguzi wa semina ya walimu wa Dini ya kiislamu iliyoandaliwa na TANZANIA ISLAMIC STUDIES TEACHING ASSOCIATION
-SEMINA YA WALIMU WATUMISHI MANISPAA YA SINGIDA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI.
Simba amesisitiza kuwa walimu wanatakiwa kujitoa na kujituma kama mitume walivyo jitoa kwajili ya kuelimisha wanadamu kuwa na maadili mema na ya kumpendeza Mungu.
Pia Sheikh Simba Amewataka Waislam nchini kuacha tabia ya kujitenga kitaasisi kwani inachelewesha maendeleo ya dini ya kiislam pamoja na kushusha maadili kwa watoto.
Katika Semina hiyo wamefundishwa mada mbalimbali zikiwemo za kutowa elimu kwa kujitoa na kujituma ili kujenga taifa lenye maadili memaa na vijana wenye kujitambua.
Wakati huo mratibu wa Semina hiyo amesema wemeamua kijiunga kwa pamoja na kuondoa makundi ili kusaidia umma wa kiislamu unao teketea kwa kukosa maarifa.
" Hizi taasisi sio chanzo cha sisi kushindwa kutoa elimu kwa vijana wetu na kulinda maadili ya kiislamu kwa vijana wetu kupitia semina hii twende tukafanye kazi ya kurudisha maadili kwa vijana wetu ili taifa liwe na vijana bora,'' Simba
Kwa upande wao walimu wameshukuru kupatiwa elimu hiyo na wemesema wanaenda kujitoa na kujituma kwa bidii ili kuwapa watoto elimu bora za kujitambua na kulindaa madili yao kama vijana wa taifa hili.
Mwisho



Post a Comment