Wakati Bongo Fleva ikiendelea kuheshimika kutoka ilipotokea hadi kufikia hii leo kuna watu mbalimbali wameweza kuipiga tafu na leo watu wanapiga bingo.
Jabir Saleh ni Mwandishi wa Habari za burudani nchi Tanzania ambaye amefanya makubwa na inapaswa apewe maua yake ili mchango wake uheshimike.
Kabla sijawataja wengine waliousaidia muziki huu kufika hapa kwanini namtaja Jabir kuupiga tafu muziki na kurudisha heshima ?
Jabir kiuhalisia anapenda sana muziki wa hip hop yaani mwanaharakati lakini hakuacha pia kusapoti muziki wa bongo flava wenyewe wagumu wanaita muziki wa "Wabana pua".
Jabir alianza kazi ya wanahabari miaka mingi lakini kupitia Times FM muongo mmoja uliopita akiwa katika kituo hiko alikuwa na kipindi kinaitwa "The Jump off" hiki kipindi kilikuwa cha mkakati na kilifanya vizuri sana alitengeneza uhusiano mzuri na wasikilizaji wake, kwa wakati huo Times FM na Clouds FM walikuwa na ushindani katika maudhui mchana kulikuwa na XXL hapa walikuwa wengi B Dozen, Adam Mchomvu, DJ Fetty yeye alikuwa jeshi la mtu mmoja The Jump Off kilianza saa mbili hadi saa nne usiku moto sana.
Baadae Times FM ikalegeza kamba haikuwa kama ile Watangazaji mashuhuri wakaanza kuondoka , Dida Shaibu, Omary Tambwe ambao wote walienda Wasafi Media, Ndimbo na wengine waliondoka katika njia hiyo Jabir Saleh naye akaondoka akaelekea E FM.
KWANINI AHESHIMIWE ?
Jabir amekuwa mbunifu katika vipindi vyake mbalimbali mbali, akaona kuna watu wanatamani kusikia yale yaliyowahi kutokea zamani katika muziki wa bongo flava.
Ndipo akaanzisha "The Classics" maudhui yake kuongelea stori za zamani za muziki wa Bongo Flava kule ulikotoka pamoja na wasanii walichokifanya
Hapo awali hakikuwepo kipindi kinachowaweka wazi wanamuziki wetu wa zamani. Inawezekana kilikuwepo lakini hakikuwa na muendelezo na mtiririko mzuri.
Mimi pia Mtangazaji na Mwandishi nasikiliza vipindi vingi kilichokuwepo ikifika Alhamis wanapiga "Throw Back Thursday" basi shughuli imeisha na wanapiga ngoma za zamani kidogo hakuna maelezo ya kina.
Kila Jumamosi pale E FM wanaitwa Wakongwe wanaelezea mambo yao, Joseph Mbilinyi A. K. A Sugu akaona hii niongezee utamu akaweka na tuzo kabisa kila mwezi kwa wasanii wa zamani kutambulika zaidi hii inatokana na harakati za Jabir Saleh.
Naamini wasanii walio wengi wa zamani watakuwa wanakitaka sana kipindi hiki wamekuja wengi juzi alikuwepo Taji Lihundi moja ya walioufikisha muziki hapa tulipo aliongea mambo mengi sana na imekuwa kama mjadala mitandaoni.
Msanii kama Nice Lucas Mkenda maarufu kama Mr Nice, Hamis Mwinjuma (Mwana FA), AY, Mr Blue , TID na wengine wengi walifika The Classics wameomgea mengi na watu wanafurahi kusikia kile ambacho kilikuwepo zamani.
Siku hizi hata katika magari yaendayo mikoani wamekuwa wakiweka mahojiano yake .
Ukiangalia namna ambavyo anakiendesha aina ya maswali hata wanahabari wa sasa wanapaswa kujifunza mengi kupitia Jabir kwanini Jabir asipewe maua yake wakati bado mzima ili ajue anachokifanya kinawapa raha watu wengi.
Taji Lihundi, Mhagama hawa wote ni miongoni mwa waliofanya muziki huu ufike hapa ulipo Bongo Flava jina hili limeasisiwa na Mhagama maua mengi kwake.
Unaweza kutoa maoni yako na ukaeleza namna ambavyo Jabir anavyokufanya ufurahie mambo ya zamani tena kwa maswali ya kisomi.
Mwisho.

Post a Comment