Nyota wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Real Madrid Antiono Rudiger ameweka wazi kuwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwake sio shida kwani anafunga huku anaendelea na kazi yake kama kawaida.
Rudiger amesema kuwa haoni shida kufunga kwani ni mwezi wa imani kwa Waislam na kufunga ni lazima hivyo anafunga na anafurahia wala hamsumbui.
"Niseme tu huu mwezi wa Ramadhani kwangu naenda nao vizuri nafurahi nafunga huku naendelea na kazi zangu," Rudiger.
Rudiger aliwahi kuitumikia Chelsea kwa mafanikio makubwa na sasa anakichapa Real Madrid na ni muumini wa dini ya Kiislam.
Mwisho.

Post a Comment