MUDATHIRI YAHYA APEWA SHAVU YANGA


 Afisa Habari wa mabingwa watetezi ligi kuu ya soka Tanzania Bara klabu ya Yanga Ally Kamwe amesema kuwa kuelekea mchezo wao dhidi ya Mamelodi Sundowns wameukabidhi kwa Mudathiri Yahya kuwa ndio siku yake.

Kamwe amesema kauli mbiu yao kuelekea mchezo huo kuwa ni "Simu ziite" wakiashiria kile anachokifanya Mudathiri baada ya kufunga goli, ameweka wazi kuwa uongozi umebariki ya kuwa mchezo huo utakuwa maalumu kwake Mudathiri kamaa ilivyo utaratibu wao. 

Aidha Kamwe ameweka wazi kuwa baadhi ya wachezaji wao ambao wapo majeruhi wameanza kupata nafuu akisema kuwa Zawadi Mauya tayari amerejea huku Yao Atoula akiwa na na asilimia 50 hadi sasa, Zouzou na Aucho wapo 80 kurejea. 

Yanga itacheza hatua ya robo fainali dhidi ya Mamelodi uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam March 30,2024.

Yanga wamekuwa na utaratibu wa kuwapa mchezo husika wachezaji wao na kwa asilimia kubwa wamefanikiwa mchezo uliopita wa klabu bingwa Afrika ulikuwa wa Pacome Zouzou ambapo Yanga walicheza na CR Belouzidad na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Post a Comment

Previous Post Next Post