Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko katika ngazi mbalimbali za uongozi, ikiwemo Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na nafasi nyingine.
Katika uteuzi huo amemteua Paul Makonda aliyekuwa katika nafasi ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) sasa amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akichukua nafasi ya John Mongela ambaye atatafutiwa kazi nyingine.
Hii inaonesha Rais Samia anaendelea kuamini anachokifanya Paul Makonda na kumpeleka kuwa mkuu wa mkoa ww Arusha mkoa ambao una mambo mengi yanayotakiwa kusimamiwa vizuri, hii ni kama amepata namba katika serikali anayoingoza Samia ili aweke nguvu zake kuusaidia mkoa uwe mahali pazuri.
Makonda aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam lakini pia aliwahi kuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na kote alifanya vizuri.
Huku Amos Makala aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza naye amepigwa Benchi angalia mkeka hapo chini.
Bado mkeka unaebdelea hapo chini angalia mabadiliko mengine.



Post a Comment