Jamii imeaswa kuendelea kusaidiana katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani lakini pia baada ya mwezi kuisha ili waweze kupata fadhila za Mwenyezi Mungu duniani na akhera.
Hayo ameyasema leo Katibu wa Bakwata mkoa wa Singida Burhan Mohamed alipoongea na Chamber Media ofisini kwake akiwaomba wale wanao toa misaada ya mbalimbali wawapatie watu husika wawape wenye mahitaji maalum.
Amesema kuwa miongoni mwa makundi ambayo yanapaswa kusaidiwa ni pamoja na Mayatima na wale ambao hawajiwezi, lakini pia amewaomba wanaofuturisha pia waangalie wale walio na mahitaji maalumu lengo la kufuturisha wapate wale ambao hawana.
"Toeni misaada kwa watu husika ambao wanashida ya kupata hiyo misaada, toeni kwa mayatima na wengine," Burhan
Sheikh Burhan ametumia fursa hiyo kuwakumbusha Waislam kuendelea kufanya ibada mbalimbali ikiwemo sunna ya swala ya TARAWEH na sunna nyingine kwani malipo yake ni makubwa mno katika mwezi huu mtukuu wa Ramadhani.
Aidha amewakumbusha mataifa mbalimbali ambayo huwa wanachinja wanyama kwa ajili ya kuwapa kiteweo wakazi wa Singida na wao wawapatie watu husika ambao wenye mahitaji maalumu.
Mwisho.
Post a Comment