Mwananchi ambaye amehojiwa TAKUKURU na kwenda kusema yaliyohojiwa ni kosa kisheria itampelekea mhojiwa kuchukuliwa hatua.
Hayo yamesemwa leo na Sipha Mwanjala Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida katika semina ya Waandishi wa Habari wa mkoani hapo juu ya maswala mbalimbali ya rushwa.
Akijibu swali la Mwandishi wa Habari wa Chamber Media Amini Nyaungo juu ya vipi elimu inatolewa kwa wananchi ili wasifanye makosa hayo baada ya kuhojiwa, Mwanjala amesema kuwa wanatoa elimu kila waendapo katika majukwaa yao pamoja na muhusika anayekuja kutoa taarifa ya rushwa anapatiwa elimu hiyo.
" Tunatoa elimu kila tukifanya matamasha yetu kupitia vyombo vya habari pamoja na muhusika anayekuja kutoa taarifa za rushwa huwa tunawaambia juu ya kusema waliyoyahoji, "
Katika mafunzo hayo pia Waandishi wa habari wameombwa kutoa taarifa pamoja na viashiria vya rushwa kuelekea uchaguzi wa Wenyeviti wa Mitaa ili uchaguzi uwe huru na haki
"Tunawaomba Wanahabari mtoe taarifa juu ya viashiria vyovyote vya rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaofanyika waka huu," amesema.
Mwisho
.jpg)
Post a Comment