Siku ya mama Tanzania iwe Samia


RAIS SAMIA SULUHU HASSAN



Inawezekana tunapokea maagizo mengi kutoka nje ya nchi lakini wala hatujashirikishwa na tunayafuata kwa ukubwa wake nitatoa mifano sahihi ya mambo hayo na kwanini tusiwe na siku ya mama ambayo tunaimiliki wenyewe na tunaiona na ikiwa na msingi mkubwa.

Siku kama "Valentine Day" inafanyika tarehe 14 mwezi wa pili kila mwaka hii siku hatujashirikishwa lakini wametoa sababu zao na inaonekana ina mantiki watu wengi wanafuata. Siku ya mama duniani, siku ya baba na siku nyingine zote wametoa vigezo vyao na tumevikubali.

KWANINI TUWE NA SIKU YETU YA MAMA TANZANIA ?

Januari 27 kila mwaka tunaazimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Samia Suluhu Hassan huyu ni kiongozi mkubwa katika ngazi ya taifa kwa mara ya kwanza anakuwa Rais mwanamke katika historia ya nchi yetu.

Kwanini tusiirasimishe iwe siku ya mama Tanzania ?, kila ikifika siku hiyo tuiweke maalumu kuwa siku yetu ya kuwaenzi kina mama, si maanishi iwe mapunziko hapana bali tuiweke kuwa siku maalumu ya mama.

Mosi tunampa heshima Rais wetu wa kwanza mwanamke kuongoza taifa hili takatifu la Tanzania, pili na sisi tumepata siku ambayo tunaiona na tunaweza kujivunia nayo kwa kutoka kwa mmoja wetu katika sisi.

Uzuri wa siku hii ni yetu na tuna historia nayo tunajua ilipoanzia wapi na kipi kimetufanya tuiheshimishe siku hii.

KWANI SAMIA KUFANYAJE HADI APEWE HESHIMA ?
Bila shaka kusingekuwa na matukio muhimu aliyoyafanya Rais Samia wala nisingefikiria kuifanya hii siku iwe ya mama.
Tuitumie kauli ya Harmonize ila tunaibadilisha  kuwa Siku ya mama sio kwa kila mtu "Mama Day is not every body" ikimaanisha kuwa anapewa heshima yule aliyefanya vizuri na Samia amefanya vizuri licha ya jukumu kubwa alilopewa kikatiba.


Hii siku nisingeiandikia kama angeboronga lakini kwakuwa amefanya vizuri basi ni sahihi kumpa heshima na kuichukua siku hii kuwa siku yetu tunayo imiliki wenyewe.

Kwa uchache makubwa aliyoyafanya kuendelea kukamilisha ujenzi wa bwawa la kufua umeme kule Rufiji  likikamilika tutapata umeme ambao utatosheleza nchi nzima maana kwa sasa tunahitaji 1600V.

Katika elimu bila shaka shule mbalimbali zimejengwa na wanafunzi wanaingia kwa mkupuo mmoja, katika afya kwa mujibu wa waziri wa Afya Ummy Mwalimu sasa hivi CTI Scan inapatikana karibuni mikoa yote lakini huduma zimeboreshwa.

Miundombinu inaenda vizuri kila mmoja shahidi huduma zamaji iko katika wakati mzuri na walio wengi wanapata maji safi na salama.

Kwanini tusirasimishe kuwa siku ya mama kila ifikapo Januari 27 hii siku iwe yetu kabisa.


Zile siju nyingine katika kalenda ya umoja wa mataifa zitaendelea kama kawaida ila hii inaingia pia katika kalenda zetu za kitaifa na inakuwa siku yetu muhimu ya kuwaenzi kina mama zetu ambao wametufanyia makubwa.

Naamini huu haina hana ya kwenda bungeni kijadili hili bali ni kitu ambacho kinawezekana kabisa wakaka hata kwa mdahalo pale ukumbi wa mwalimu Nyerere na ikapita hii ikawa katika sehemu sahihi ya kutambulika.

Haya ni mawazo ambayo kila mmoja anaweza akawaza ila kuna mawazo mengine yanaeleweka na kuleta tija  kwanini tuheshimishe siku ya watu wakati yetu ipo vizuri na inaelezeka na tunaweza kuipambania ikaingia katika kalenda ya kimataifa tukifanya uchunguzi katika ngazi hizi hasa Rais wanawake Afrika wako wangapi na viongozi wa ngazi za juu tukaunganisha kwa pamoja na tukazitetea hoja zetu huenda ikaingizwa katika kalenda za kidunia. 

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post