WATU WAZIMA ACHENI KUTUMIA DAWA ZA MENO ZA WATOTO, JALI AFYA YAKO YA KINYWA NA MENO

 Na Dokta Baraka Nzobo



Kagua dawa yako ya meno hapo nyumbani.

Kama total fluoride contents ni 1000 ppm hiyo ni ya watoto wa umri wa miaka 0-5. Hawa wana meno ya kitoto tu.


Kuanzia umri wa miaka 6 -100+ unatakiwa utumie dawa ya meno yenye Total Fluoride contents kuanzia 1450-1500ppm. Kundi hili lina watoto ambao wameshaanza kuotesha meno ya ukubwani na pamoja na sisi watu wazima ambao tuna meno yote ya ukubwani.

Kaba ya kununua dawa ya meno angalia nje kwenye box la hiyo dawa upande wa nyuma kuna maandishi mengi sana, nenda sehemu imeandikwa *CONTENTS*  au *INGREDIENTS* angalia neno SODIUM FLOURIDE  (utaona kiasi kilichopo kati ya 1000ppm au 1450ppm). Maandishi hayo yanatakiwa kuwepo na kwenye tube ya ndani inayobeba dawa. 1000ppm ni kwa watoto na 1450-1500ppm ni kwa watu wazima.



Meno ya watoto wenye miaka 0-5 yanalindwa vizuri  kwa dawa ya meno yenye fluoride ya 1000ppm.

Meno ya ukubwani yanalindwa vizuri  kwa dawa ya meno yenye fluoride ya 1450-1500ppm.


Fluoride ndiyo madini yanayosaidia kuimarisha gamba la nje la jino lisitoboke au kuoza. Ukitumia dawa ya meno yenye kiwango sahihi cha fluoride kwa meno yako utakuwa na uhakika wa kuwa na meno salama (hayataoza au kutoboka)


Wizara ya Afya hatutaji MAJINA YA KAMPUNI ZA DAWA ZA MENO kufanya hivyo ni KOSA KISHERIA, tuna kuhimiza kabla ya kununua dawa ya meno ikague kama imeandikwa hivyo viwango tunavyovisema, ni kazi ya dakika 1 tu. 



Watanzania tujenge utamaduni wa kusoma vitu tunaponunua madukani. Usiposoma utakuja uziwa hadi bidhaa zilizokwisha muda wake wa matumizi (Expiry).


Mwenye masikio na asikie na Mwenye macho na aone.


WEWE NI MTU WA  THAMANI SANA.

Post a Comment

Previous Post Next Post